1 Februari 2019 - 06:41
Umoja wa Ulaya waingilia mambo ya ndani ya Venezuela

Bunge la Ulaya limepiga kura ya kumtambua Juan Guaido aliyejitangaza binafsi kuwa rais wa mpito nchini Venezuela na kumupinga rais aliyechaguliwa kihalali na wananchi Nicolas Maduro, hatua hii inaonyesha wazi jinsi Ulaya isivyochunga na kuheshimu mipaka ya nchi nyingine.

Shirika la habari la ABNA linaripiti kuwa: Bunge la Ulaya limepiga kura ya kumtambua Juan Guaido aliyejitangaza binafsi kuwa rais wa mpito nchini Venezuela na kumupinga rais aliyechaguliwa kihalali na wananchi Nicolas Maduro, hatua hii inaonyesha wazi jinsi Ulaya isivyochunga na kuheshimu mipaka ya nchi nyingine.

Wabunge wa Umoja wa Ulaya walipiga kura 429 kumuunga mkono Guaido dhidi ya 104 waliopinga udhalimu huo, huku 88 wakijizuia kupiga katika kikao maalum mjini Brussels. Kura hiyo ni ya kiishara tu, kwa sababu bunge hilo halina usemi katika sera ya kigeni ya Umoja wa Ulaya. Bunge hilo limetoa wito kwa mataifa 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya kumtambua Guaido kuwa kaimu rais halali wa Venezuela hadi pale uchaguzi mpya wa rais ulio huru, uwazi na wa kuaminika utakapoandaliwa

Katika mahojiano yaliyochapishwa leo na gazeti la Uhispania la El Pais, Guaido amefutilia mbali uwezekano wa kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini mwake, akisema kuwa wananchi wengi wanamtaka Maduro ajiuzulu. Kiongozi huyo wa bunge la Venezuela ameurudia wito wake kwa jeshi la nchi hiyo kumuunga mkono.

Alijiapisha Januari 23, akisema katiba inamruhusu kuhudumu kama kiongozi wa taifa kwa sababu uchaguzi wa Maduro mwezi Mei mwaka jana haikuwa halali kwa vile wapinzani wake wakuu walijitoa kugombea.

Nayo Urusi, ambayo inamuunga mkono Maduro, imesema leo kuwa iko tayari kusaidia kusimamia mazungumzo ya upatanishi kati ya Maduro na upinzani nchini Venezuela.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Urusi Maria Zakharova amevitaja vikwazo vya Marekani dhidi ya Venezuela kuwa "kitendo halisi cha hujuma”

Ni Marekani tu na nchi kadhaa za Amerika Kusini zilizomtambua Guaido kuwa rais wa Venezuela. Mataifa sita ya Umoja wa Ulaya – Uhispania, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Uholanzi na Ureno – zimesema zitamtambua Guaido kuwa rais kama Maduro hatoitisha uchaguzi mpya ifikapo Jumapili wiki hii.

Rais Maduro amepinga mashart ya Ulaya na kusema kuwa hawana haki ya kutoa maamuzi katika nchi nyingine.

Mwisho wa habari / 291